Monday, September 30, 2019

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

ORODHA YA MAJINA WANAOTAKIWA KUSAHIHISHA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020


HESLB imetoa orodha ya waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zina upungufu ili wafanye marekebisho kwa siku nne kuanzia leo Jumatatu ambapo pia mwongozo wa jinsi ya kufanya marekebisho utatolewa..

Hatua ya HESLB inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo imebainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.

Orodha hii ni ya wanafunzi wanaokwenda kusoma masomo ya Shahada ya kwanza. Orodha ya waombaji mikopo watakaojiunga na Shule ya Sheria (Law School of Tanzania), Shahada za Uzamili na Uzamivu

Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika *bofya hapa.*

Monday, September 09, 2019

Tanzania Yatinga Hatua Ya Makundi kujiandaa kushiriki kombe la dunia

Tanzania Yatinga Hatua Ya Makundi kujiandaa kushiriki kombe la dunia
Hatimaye Taifa stars yatinga hatua ya Makundi baada ya hapo jana kuifunga Burundi ktika ngazi ya penati,katika kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 kwa ushindi wa penati 3-0 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa marudiano uliomalizika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.huku katika upande wa taifa stars ikishinda penati zote na burundi kukosa penati zote.hongereni Taifa stars,hongereni Tanzania kwa ushindi mzito.