Tuesday, July 25, 2017

KUJIUNGA NA DEGREE NIT ONLINE ADMISSION

BONYEZA HIYO LINK HAPO CHINI KWA KUJIUNGA NA NATIONAL INSTITUTE OF TRASPORT (NIT) KWA COURSE MBALIMBALI NGAZI YA DEGREE

 NIT OAS

MIFANO:
  • Human Resource Management
  •  Business Administration
  • Marketing and Public Relations
  •  Accounting and Transport Finance
  •  Aircraft Maintenance Engineering
  •  Education with Mathematics and Information Technology
  • Automobile Engineering
  • Mechanical Engineering
  • Procurement and Logistics Management
  • Information Technology
  • Computer Science
  • Logistics and Transport Management                 
NIT OAS 





HESLB yajipanga maombi ya mikopo 2017/2018

HESLB yajipanga maombi ya mikopo 2017/2018

Wakuu na maafisa wa Idara na Vitengo mbalimbali vya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  wapo katika maandalizi ya mwisho ya kufanyia majaribio mfumo wake ulioboreshwa wa uombaji mikopo kupitia  olas.heslb.go.tz kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa TEHAMA Bw. Muze Ninkhambazi ambaye ameongoza mafunzo ya kuwapitisha idara na vitengo hivyo ili kuufahamu na kupata mapendekezo kutoka kwao kwa ajili ya kuboresha mambo muhimu yanayoingia katika mfumo huo kabla ya kukaribisha maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Bw. Ninkhambazi amesema mabadiliko ya mfumo yanalenga kuufanya uwe wa kisasa zaidi na kuwarahisishia waombaji mikopo jinsi ya kuwasilisha taarifa zao Bodi. Aidha ameongeza kuwa maandalizi hayo yamewezesha kupata mchango mkubwa kutoka wa washiriki.

Miongoni mwa mabadiliko katika OLAMS ni pamoja na jinsi ya kufanya malipo, kuwasilisha viambatanisho muhimu kama cheti cha kuzaliwa, cheti cha kidato cha nne na saini za mwombaji na mdhamini wake.
Bodi ya Mikopo iliingia katika mfumo wa uombaji mikopo kwa njia ya mtandao mwaka wa masomo 2010/2011 na tangu wakati huo mfumo huo umekuwa ukiboreshwa ili kuendana na teknolojia mpya.

Thursday, July 20, 2017

Kuongezwa kwa muda wa uhakiki wa wanafunzi wanaotegemea kwenda vyuo.

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa muda wa kufanya maombi ya uhakiki wa tuzo zao umeongezwa hadi tarehe 15 Agosti 2017.


Hivyo kwa wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao hawajaomba na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki.


Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kufanya uhakiki wa tuzo zao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho wa muda wa uhakiki.


Hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya Tarehe tajwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 19/07/2017

Sunday, July 16, 2017

ANGALIA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2017












Kuangalia Matokeo ya Form six 2017/18 bonyeza hapo chini
Matokeo ya Form Six 2017/18


Kuangalia Matokeo ya Form six 2016/17 bonyeza hapo chini
kuangalia Matokeo Ya Form six 2016 bonyeza hapa


Kuangalia Matokeo ya Form six 2015/16 bonyeza hapo chini
Matokeo ya Form six 2015/16

Kuangalia Matokeo ya Form six 2014/15 bonyeza hapo chini
Matokeo ya Form Six 2014/15
                                                 
Kuangalia Matokeo ya Form six 2013/14 bonyeza hapo chini 
Matokeo ya Form six 2013/14
                          
Kuangalia Matokeo ya Form six 2012/13 bonyeza hapo chini
Matokeo ya Form six 2012/13