Tuesday, November 15, 2016

Orodha ya vyuo 26 vilivyofutiwa usajili na NACTE leo

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika cheti cha usajili wa vyuo hivyo, huku likisimamsisha utoaji wa programu zilizokuwa zikitolewa katika vyuo 20 ambazo hazijasajiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.
 
Katibu huyo amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.
NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania.  Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.
 
Hapa chini ni mgwanyo wa vyuo katika makundi matatu na hatua zilizochokuliwa dhidi ya kila kundi
 
Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili
S/N CHUO
1 Institute of Management and Development Studies – Iringa
2 Green Hill Institute – Mbeya
3 Institute of Business and Social Studies – Mbeya
4 Loyal College of Africa – Mbeya
5 Mbeya Training College – Mbeya
6 Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga
7 New Focus College – Mbeya
8 Shukrani International College of Business and Administration –  Mbeya
9 Majority Teachers College – Mbeya
10 Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga
11 MAM Institute of Education – Mbeya
12 Belvedere Business and Technology College – Mwanza
13 Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita
14 Global Community College – Geita
15 Muleba Academy Institute – Muleba
16 St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita
17 Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza
18 Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza
19 Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam
20 SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam
21 Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara
22 Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha
23 Emmanuel Community College – Kibaha
24 Modern Commercial Institute – Dar es Salaam
25 Marian College of Law – Dar es Salaam
Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa
S/N CHUO MAFUNZO
1 MISO Teachers College – Mafinga Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
2 Tusaale Teachers College – Mafinga Competence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
3 The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro
4 The Golden Training Institute – Dar es Salaam





5 Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma
6 National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha
7 Musoma Utalii Training College – Musoma
8 Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza
9 Mwanza Polytechnic Institute – Maswa
10 Ruter Institute of Financial Management – Mwanza
11 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza
12 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita
13 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba
14 Singni International Training Institute – Bukoba
15 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama
16 Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu
17 Richrise Teachers College – Geita
18 Twiga Training Institute – Musoma
19 Zoom Polytechnic Institute – Bukoba
20 St. Thomas Training College – Shinyanga
Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi
S/N CHUO
1 MISO Teachers College – Mafinga
2 Rungemba Teachers College – Mafinga

Friday, November 11, 2016

MAREHEMU SAMWEL JOHN SITTA AAGWA BUNGENI

Baadhi ya picha mbalimbali za kuagwa kwa MAREHEMU SAMWEL JOHN SITTA




Bodi ya mkopo

bodi ya mikopo ya elimu ya juu imeanza kuongeza majina ya wanafunzi wa elimu ya juu waliopata mikopo mwaka wa masomo 2016/2017,pamoja na kupanga distribution ya mkopo aliopata kila mwanafunzi(%).
KUANGALIA MKOPO WAKO 
bonyeza Hapa

Hotuba ya Zitto Kabwe ...msiba wa M.MH S sitta

Tangulia Spika wa watu, Tangulia Spika Bunge la Wananchi

Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto katika Kikao Maalumu cha Bunge cha Mazishi ya Spika Mstaafu, Samwel John Sitta

Ndugu Spika,
Ndugu Wabunge,
Mama Magreth Sitta,
Watoto wote wa Mzee Samwel John Sitta, Ndugu, Jamaa na Marafiki,
Ndugu zangu Watanzania,

Leo kikao maalumu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wake wa Tano kinamuaga mtoto wa Mzee John Sitta na Hajjat Zuwena Said Fundikira. Nami nimepewa nafasi niseme maneno machache juu ya muagwa wetu huyu.

John Samwel Sitta anayo mengi, lakini Tanzania itamkumbuka kama mtu aliyejaribu kuboresha kila alichokabidhiwa kama jukumu, shujaa wa wote wanaoamini katika Uwajibikaji wa kitaasisi, Mwanasiasa aliyepanda na kushuka na kisha kupanda na kubakia kileleni, taswira ya mkoa wake wa Tabora, sio tu mdhamini wa klabu ya Simba, bali pia Mwanasimba aliyeipeleka klabu Brazil na kuwezesha kuifunga Yanga mabao mengi zaidi ambayo hayajapata kulipwa na wapinzani wetu hata kwa kuungakuunga, Mwanamageuzi wa Bunge na Spika wa mioyo ya Watanzania.

Hata katika kifo chake, Samwel John Sitta ameweka rekodi nyengine - kwa Bunge kufanya kikao maalumu kuenzi mmoja wa wajumbe wake mahiri kati ya mwaka 1975 - 2015 isipokuwa tu kwa kipindi cha 1995 - 2005. Rekodi hii itaendelea kwa wengine wote watakaofuata baada yake.

Ni mtu wa namna gani wewe Samwel Sitta? Spika wa Kasi na Viwango, unayeweka rekodi hata ukiwa umelala ndani ya Jeneza lako lililopambwa na Bendera ya Taifa letu ukielekea nyumbani kwako Urambo kwenye nyumba yako ya milele. Ulikuwa hushindwi ukiwa hai, umeonyesha umahiri wako hata ukiwa kwenye umauti. Kweli wewe ni Spika wa Watu (The Peoples Speaker).

Tuliokupenda tunajua. Ulikuwa Baba mlezi. Ulikuwa Mume mwema. Ulikuwa Babu. Ulikuwa Kiongozi. Nadhani hata kwa uliokwaruzana nao hapa na pale wanajua hilo. Leo sote tuna majonzi makubwa. Umeliunganisha Taifa katika kukukumbuka ewe Spika wa Watu.

Ulikuwa na vyeo vingi; Mbunge, Naibu Waziri, Waziri, Mkuu wa Mkoa, Waziri tena, Mkurugenzi Mtendaji, Spika, Waziri tena na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba. Lakini, wala, tunakuita Spika Sitta tu. Kwanini? Kwa sababu 'Legacy' yako ni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sio kwamba umeanzisha Bunge wewe, la hasha. Lakini ulipopokea Uspika wa Bunge letu, kama ilivyo jadi yako, uliliboresha, uliwezesha kutunga kanuni mpya, uliimarisha Mhimili huu na kuuweka katika nafasi yake ya Kikatiba.

Nakumbuka siku moja ulimwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aongee na baadhi yetu, ilikuwa mwaka 2006. Mimi nikiwa nina miaka 29 tu. Tukakutana na Rais ukumbi wa Msekwa. Baada ya kikao kilichofanikiwa kumshawishi Rais kuhusu mabadiliko uliyoyataka uliniambia;

"Babu, mimi sasa alasiri, ninyi ndio saa nne asubuhi. Nawawekea misingi tu na kuliweka Bunge katika nafasi yake ya kikatiba".

Kilichofuata ni mabadiliko makubwa ya Kanuni za Bunge, kuandikwa upya kwa Sheria ya Bunge (National Assembly Administration Act, 2008) na kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Majimbo, Constituencies Development Catalyst Fund (CDCF).

Samwel Sitta, bado tunasikia mwangwi wa sauti yako nene kutoka kwenye kiti cha Spika ukiwataka Mawaziri wajibu maswali kwa ufasaha. Hukuisahau Tabora yako. Damu ya kichifu wa Unyanyembe ya Fundikira kutoka mama yako Zuwena ilikusambaa kwenye mishipa yako. Ukiona kuna swali linalohusu mkoa wako wa Tabora hukusita kuwaambia Mawaziri wajibu vizuri (haswa kuhusu barabara), au ukiamsha jeshi lako (akina Lucas Lumambo Selelii nk) wakisema "mheshimiwa Spika, wewe leo ukipata dharura Urambo unafikaje!". Yote hiyo kutilia nguvu umuhimu wa maendeleo ya mkoa wako.

Wewe ni kielelezo cha Demokrasia ya Vyama vingi bungeni. Ulitoa nafasi kwa wabunge wote wa kambi zote ndani ya Bunge. Hatusemi hukubagua, la hasha, uCCM wako ulikuwa pale pale. Lakini walio wengi walishinda na walio wachache walisikika. Ndio Demokrasia hiyo.

Sitta ulikuwa Muungwana. Nakumbuka siku ile unamwomba radhi Mzee John Momose Cheyo katika kamati ya Uongozi (baada ya kuwa ulimtoa kwa makosa bungeni), eti msongo wa mawazo ulikujaa kwani watu wanapitapita Jimboni. Lakini uliwashinda. Unyenyekevu wako wa kuomba radhi unapokosea ni somo kubwa sana kwa Viongozi wengine tuliobakia.

Wabunge wenzangu, tunataka kumuenzi Spika wa Watu - Samwel John Sitta? Basi hakuna kumuenzi bora zaidi kama kuimarisha uhuru na heshima ya Bunge letu.

Tuendeleze Jahazi.

Samwel Sitta anakwenda kwenye nyumba yake ya milele akiongozwa na imani yake kubwa kwa Mungu na uzalendo wake usio na mawaa kwa nchi yake Tanzania. Angalau bado ataendelea kuwa nasi kwa kutuachia mafundisho makubwa kutokana na Maisha yake, mambo mema aliyoyafanya kwa nchi yetu, ndoto aliyoiishi ya Tanzania imara na yenye heshima, na malezi kwa viongozi wengi vijana aliowafunda na kuwalea kiuongozi.

Ni dhahiri umeishi maisha yako Babu. Kama isemavyo biblia, 2 Timotheo 4:7 "Nimepigana Vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda".

Tangulia Spika wa Watu (The Peoples’ Speaker).Tangulia Spika wa Bunge la Wananchi. Tangulia Samwel John Sitta.
Mola akulaze pema.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Novemba 11, 2016
Dodoma

Thursday, October 27, 2016

Monday, October 17, 2016

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NIT 2016/2017


 
Kuona Majina bonyeza hapa

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WA CHUO CHA MAJI UBUNGO WALIOPATA MKOPO 2016/2017

Names of WTF Loan Beneficiaries 2016-17

ATTENTION TO THE WTF LOAN APPLICANTS
The Board of The Registered Trustees of Water Technicians Fund (RTWTF) hereby wishes to inform all loan applicants that by applying and meeting the loan allocation criteria, eighty eight (88) applicants have qualified to be beneficiaries of the loan
for the academic year 2016/2017. The Board likewise disqualified some of the applicants for not adhering to the instructions laid in the form as well as not putting either valid certificates or the required attachments. The board went further to verify the information provided by applicants. The list of successful applicants can be viewed on this website under Publications.
kuona majina hayo bonyeza hapa

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MWAKA WA MASOMO 2016/2017-FIRST BATCH

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017 awamu ya kwanza.
 kuona Majina hayo bonyeza hapa
Majina ya mikopo First Batch

Mamia ya watu wamiminika kumwaga Dkt. Didas Masabur

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016




Saturday, October 01, 2016

Simba vs Yanga

Leo ndio ile mechi iliyokuwa inasubiliwa kwa hamu kati ya timu kongwe mbili, simba na yanga



Monday, September 26, 2016

Haya hapa majina ya udom

The University of Dodoma (UDOM) wishes to announce the names of candidates selected for admission into various undergraduate programmes for the academic year 2016/17.


Admission letters for successful candidates are will be available soon.

to download click here:

SELECTED-CANDIDATES-TO-JOIN-VARIOUS-UNDERGRADUATE-DEGREE-PROGRAMMES-FOR-ACADEMIC-YEAR-2016.2017 

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU MWALIMU NYERERE 2016/2017

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU MWALIMU NYERERE 2016/2017

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA UNIVERSITY 2016/2017

 MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU TUMAINI MAKUMIRA UNIVERSITY 2016/2017
 makumira-tcu-selection-2016-2017

Undergraduate Admission degree Programme 2016/2017

Undergraduate Admission degree Programme 2016/2017


The following applicants have been selected to join various undergraduate degree programmes for the 2016/2017 academic year. The selected applicants should report at the Mwl. J.K. Nyerere Mlimani Campus on Saturday 8th October 2016 for the orientation week which will start on Monday 10th October 2016. Applicants selected for admission into Dar es Salaam University College of Education (DUCE) and Mkwawa University College of Education (MUCE) should report directly to the college's campuses in Chang'ombe and Iringa respectively on the same dates. Joining instructions and admission letters should be collected at the University campuses where one is admitted. Joining instructions and other important information can also be downloaded from the University website
Udsm
Udsm admission 2015/2016 

Sunday, September 18, 2016

Serikali kutoa ubani kwa wafiwa wa tetemeko Bukoba

SERIKALI imesema itatoa fidia ya Sh milioni 1.17 kwa kila familia iliyofiwa na ndugu wakati wa tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu mkoani Kagera.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alipokuwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne wa Bunge la 11.
“Kama Bunge lako tukufu lilivyojulishwa, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, imechukua hatua kadhaa kushughulikia athari za tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10, mwaka huu.
“Pamoja na viongozi kutembelea maeneo yenye madhara, Serikali pia imewapatia chakula waathirika, imeimarisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kupeleka dawa na vifaa tiba kupitia Bohari Kuu ya Dawa na pia imepeleka timu ya wataalamu na madaktari 12 kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.
“Wananchi waliokosa kabisa hifadhi ya makazi, wamepewa maturubai na mahema kwa ajili ya makazi ya muda na waathirika ambao nyumba zao zimebomoka kabisa kwa kuanzia kila mmoja ametengewa mabati 20, saruji mifuko mitano pamoja na mablanketi na mikeka na kwa wapangaji waliokuwa katika nyumba hizo kila mmoja ametengewa kodi ya pango ya miezi sita ili apate mahali pa kujihifadhi.
“Tathmini ya uharibifu wa barabara imefanyika na barabara zilizoharibika zitarejeshwa katika hali yake ya kawaida ili wananchi waendelee kupata huduma za msingi huku Serikali ikiendelea kuchukua hatua za kukarabati miundombinu ya maji safi na maji taka.
“Pamoja na hayo, Serikali imewafariji wafiwa na kushiriki mazishi kwa kusaidia kutoa majeneza, sanda, usafiri na kutenga shilingi milioni 20 za rambirambi kwa wafiwa ambazo zitatolewa kwao muda wowote,” alisema Majaliwa.
Pia alizungumzia mwenendo wa ukusanyaji wa mapato serikalini na kusema Serikali imedhamiria kuongeza na kuimarisha ukusanyaji huo kwa kuchukua hatua mbalimbali.
Katika hatua nyingine, alisema katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, mapato ya Serikali yanatarajia kuongezeka na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka kwa washirika wa maendeleo huku ikiendelea kudhibiti utoaji wa misamaha ya kodi ili kuleta tija kwa Taifa.
“Katika mwaka wa fedha wa 2016/2017, Serikali imelenga kukusanya mapato ya ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri ya jumla ya shilingi trilioni 18.46. Takwimu za mwenendo wa ukusanyaji wa mapato zinaonyesha kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Agosti, mwaka huu, mapato yaliyokusanywa na TRA yalikuwa shilingi trilioni 2.168 ikilinganishwa na makadirio ya kukusanya shilingi trilioni 2.113,” alisema.

TCU yashusha viwango kujiunga vyuo vikuu

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imetangaza kushusha viwango vya kujiunga na elimu ya juu (GPA) kwa wahitimu wa ngazi ya stashahada kutoka 3.5 hadi 3.0.
Bila kueleza sababu ya kufikia uamuzi huo, TCU imesema kushushwa kwa viwango hivyo kumelenga kuruhusu idadi kubwa ya wanafunzi kudahiliwa katika vyuo vikuu mbalimbali nchini, huku vigezo vingine vikisalia kama vilivyokuwa awali.
Pamoja na hilo, TCU pia imeongeza muda wa udahili kuanzia Septemba 12 hadi 23 mwaka huu ili kutoa fursa kwa waombaji wenye sifa kuchagua tena kozi zenye nafasi baada ya zile walizoomba awali kujaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Eleuther Mwageni, alisema jumla ya walioomba nafasi katika awamu ya kwanza ni 55,347.
Alisema katika awamu hiyo iliyohusisha wanafunzi kutoka kidato cha sita na wenye vyeti kutoka nje ya nchi jumla ya waliodahiliwa ni 30,731 ambapo kidato cha sita ni 30,529 huku wenye vyeti kutoka nje ya nchi wakiwa ni 202.
Waliokosa nafasi katika awamu ya kwanza ni 24,616 ambapo 24,341 ni wale waliohitimu kidato cha sita na 275 ni wenye vyeti kutoka nje ya nchi.
Alisema katika jumla ya waombaji 55,347 walioomba wenye sifa za kudahiliwa ni 47,203 sawa na asilimia 85.3% waliopata ni 30,731 sawa na asilimia 65% waliokosa ni 16,472 sawa na asilimia 35% na wasiokuwa na sifa ni 8,144.
Mwageni alisema wengi waliokosa ni kutokana na kujaa kwa nafasi katika vyuo walivyoomba ambapo idadi kubwa ya waombaji kupendelea zaidi vyuo hivyo.
“Kwa mfano kozi zote zinazotolewa na Muhimbili na nyingi za Chuo cha Ardhi zimejaa, baadhi ya kozi zimekimbiliwa na waombaji wengi kuliko nafasi zilizopo katika vyuo hivyo,” alisema Mwageni.
Alizitaja kozi nyingine zilizojaa katika vyuo vilivyoombwa na idadi kubwa ya waombaji kuwa ni ualimu, udaktari wa binadamu, ufamasia, sayansi ya uthamini wa ardhi na sheria.
“Kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam ilikuwa na waombaji 15,803 wakati nafasi ni 1,000 tu. Halikadhalika kozi ya sayansi ya uthamini wa ardhi ya Chuo Kikuu Ardhi ilikuwa na waombaji 4,599 wakati nafasi ni 100,” alieleza Mwageni.
Aliongeza kuwa waliokosa nafasi ni kutokana na ushindani uliopo kutokana na uhaba wa nafasi katika kozi hizo huku baadhi ya waombaji wakishindwa kuzingatia sifa linganishi.
“Kwa hali hiyo Tume imeongeza muda wa udahili kuanzia Septemba 12 hadi 23 mwaka huu kwa waombaji wenye sifa ili wapate fursa ya kuchagua tena kozi zenye nafasi,” aliongeza Mwageni.
Mapema Julai mwaka huu, Tume hiyo ilitangaza kuongeza viwango vya kujiunga na elimu ya juu kwa wanafunzi waliohitimu ngazi ya stashahada kutoka  GPA 2.7 iliyokuwapo awali hadi 3.5.

Friday, July 15, 2016

Monday, July 04, 2016

Mabasi ya haraka kuanza kutumia gesi




MSIMAMIZI wa Usambazaji Gesi katika Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Ismail Naleja, amesema awamu ya pili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam yatatumia nishati ya gesi asilia badala ya mafuta jambo litakalosaidia kupunguza gharama. Katika awamu ya pili, mabasi mapya 200 ya mradi huo yanatarajiwa kuingizwa nchini.
Akizungumza katika Maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kuhusu usambazwaji wa gesi katika magari, Naleja alisema hatua hiyo itaongeza idadi ya magari yanayotumia gesi nchini ambapo hivi sasa kuna mabasi 60 yanayotumia gesi na kuwashauri wenye magari kutumia mfumo huo ili kupunguza gharama za uendeshaji.
“Uendeshaji wa gesi utakuwa nafuu jambo linaloweza kufanya hata nauli zake kupungua kwani kilo moja ya gesi inatumika katika umbali unaotumiwa na mafuta ya dizeli lita moja na nusu,” alieleza Naleja.
Alisema kilo moja ya gesi ni Sh 1,500 wakati lita moja na nusu ni Sh 3,000, pia gesi haiharibu mazingira kwa sababu haina kaboni ikilinganishwa na petroli.
Aliongeza kuwa, gharama ya ufungaji wa mfumo wa gesi kwenye gari ni Sh milioni mbili, fedha ambayo inarudi baada ya kupunguza gharama katika matumizi kwa miezi mitano tu.
Mtaalamu huyo alisema matumizi ya gesi katika magari si hatari, kwani gesi inayotumika ni nyepesi kuliko inayotumika majumbani, hivyo ikivuja inasambaa hewani na tatizo likitokea mtungi wa gesi unajifunga.
Naye Msemaji wa Kampuni inayoendesha mabasi ya haraka ya UDART, Sabri Mabrouk alisema ni kweli kuwa awamu ya kwanza ya magari yaendayo haraka hayakuweza kutumia gesi kutokana na shirika hilo kuchelewa kupeleka wazo hilo. Hata hivyo sasa wameshafanya mazungumzo ili mradi wa awamu ya pili utumie gesi ili kupunguza gharama.
Alisema wanatarajia awamu ya pili ya mradi utakuwa na mabasi 200.

Kesi za mafisadi kutozidi miezi 9

JAJI Mkuu, Mohammed Chande Othman, amesema Mahakama Maalumu ya Uhujumu Uchumi na Ufisadi itaamua kesi kwa muda usiozidi miezi tisa na kwamba itaanza na majaji 14.
Aidha, wameandaa kozi maalumu kwa majaji 14 watakaofanya kazi katika mahakama hiyo itakayoanza Julai 11 hadi 15, mwaka huu, kwenye Chuo cha Mahakama Lushoto mkoani Tanga, ili kupeana mwongozo juu ya uendeshaji wa mahakama hiyo.
Jaji Mkuu alisema, kesi zitakazoendeshwa katika mahakama hiyo ni zile ambazo upelelezi wake umekamilika ili uamuzi utolewe mapema. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kupambana na uhalifu huo.
Aliyasema hayo jana wakati alipotembelea Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo katika Barabara ya Kilwa, ambayo alisema yamezidi kuwa bora kuliko miaka mingine. Alisema baada ya sheria hiyo ya uhujumu uchumi kupitishwa na Bunge, imekuwa na marekebisho mengi na kuboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Jaji Mkuu alisema pia, hatua inayofuata ni Rais kutoa idhini ya sheria hiyo na baadaye kupitishwa kwa kutangazwa katika Gazeti la Serikali ili ianze kutumika.
Alieleza kuwa baada ya kutangazwa katika Gazeti hilo la Serikali, Jaji anatakiwa kutunga kanuni mbalimbali, mojawapo ikiwa ya kulinda mashahidi kutokana na kuwa sheria hiyo inahusu makosa makubwa na hatari ya ugaidi, rushwa na uhujumu uchumi.
“Tuko mbioni kutunga kanuni hizo na kuhakikisha mashahidi wanalindwa. Jengo la mahakama hii litakuwa katika Chuo cha Sheria karibu na Mlimani City na tayari tumepeleka wasajili watendaji,” alisema.
Mwishoni mwa wiki, Jaji Mkuu huyo alisema kuwa majengo ya mahakama hiyo yatakabidhiwa leo. Kutokana na maelezo yake, Mahakama iko tayari kuendesha divisheni hiyo, baada ya kukabidhiwa majengo hayo.
Alisema wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo juu ya namna divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake. Aidha, aliweka wazi kuwa hadi sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.

Wednesday, May 25, 2016

Yanga vs TP Mazembe

KITENDAWILI cha makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF CC) kiliteguliwa jana, ambapo wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo Yanga wamepangwa kundi moja na mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Upangaji wa ratiba hiyo ulifanyika jana mjini Cairo, Misri, ambapo TP Mazembe ni timu yenye umaarufu Tanzania, ambapo nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ambaye kwa sasa anachezea KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta alitokea timu hiyo kabla ya kwenda Ulaya mwaka huu.
Pia Mazembe ni timu anayochezea Mtanzania mwingine, Thomas Ulimwengu anayechezea pia Taifa Stars na tangu mwaka 2011 ilipokuja nchini kucheza na Simba katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ilitokea kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki.
Katika droo ya CAF jana mchana, Yanga imepangwa Kundi A na Mazembe, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana na ratiba inaonesha mechi za makundi zitaanza Juni 17 mwaka huu. Kwa upande wa Kundi B zipo timu za Kawkab Athletic, Fath Union Sports zote za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisia na Ahly Tripoli ya Libya.
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa, Zesco ya Zambia imepangwa kundi moja na Al Ahly ya Misri, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Wac ya Morocco. Kundi B lina timu za Enyimba ya Nigeria, Zamalek ya Misri, Es Setif ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Yanga iliingia makundi ya michuano hiyo baada ya kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, ambapo iliangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.
Ilianza vizuri Ligi ya Mabingwa kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
Wakati huo huo, awali jana Kamati ya Maandalizi ya michuano ya klabu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeiondoa AS Vita ya DRC kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kosa la kumtumia mchezaji Idrissa Traore hatua za awali akiwa anatumikia adhabu.
Kamati hiyo imefikia uamuzi huo katika kikao chake mjini Cairo, baada ya kupitia malalamiko ya klabu ya Stade Malien ya Mali dhidi ya As Vita juu ya Idrissa Traore.

Thursday, May 05, 2016

Fainali ni mardid vs atletico 2016

 mardid na atletico wamefanikiwa kuingia Fainali ya ligi ya mabingwa ulaya itakayochezwa mei 28 katika jiji la milani italia

Friday, April 29, 2016

Rais Magufuli amtumbua Mkurugenzi Mkuu TIC

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki kwa sababu mbalimbali, ikiwemo kutochukua mshahara wake tangu alipoteuliwa mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, Dk Magufuli ametengua uteuzi huo rasmi kuanzia Aprili 24, mwaka huu. Profesa Mkenda alisema pamoja na mambo mengine, hatua hiyo imechukuliwa na Dk Magufuli baada ya kupata taarifa kuwa mkurugenzi huyo alikuwa hachukui mshahara wa serikali tangu alipoajiriwa, jambo lililozua maswali.
Aidha, kwa mujibu wa Profesa Mkenda, endapo Kairuki atakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na Serikali ya Awamu ya Tano, atapangiwa kazi nyingine. Alisema kutokana na hatua hiyo, tayari mchakato wa kumpata Mkurugenzi mpya umeanza mara moja.
“Wakati mchakato huo ukiendelea kwa sasa Clifford Tandali atakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo. Kairuki anakuwa Mkurugenzi wa pili wa mashirika ya umma kutenguliwa uteuzi wake baada ya Rais Magufuli juzi kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Ally Simba.
Kairuki ni mtaalamu wa Sheria na masuala ya ubia kati ya Serikali na wawekezaji, na aliteuliwa kushika wadhifa huo Aprili 12, 2013 na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kutoka katika Chama cha Mabenki Afrika Kusini akiwa ni Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha.

Thursday, April 21, 2016

Meya Chadema aomba Rais Magufuli aungwe mkono

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema) amesema ni wakati wa kuweka itikadi za siasa pembeni na kumuunga mkono Rais John Magufuli katika jitihadi zake za kuijenga nchi.
Pamoja na hayo, mameya wa manispaa mbalimbali za jiji hilo, wamebainisha kuwa wamepanga kufanya kazi kwa ushirikiano kwa lengo moja la kulijenga jiji hilo na kuwaletea wananchi wake maendeleo bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Akizungumza katika uzinduzi wa daraja la kisasa la Nyerere jijini Dar es Salaam juzi, Mwita alisema kwa sasa Tanzania inahitaji umoja na mshikamano. “Baada ya harakati za uchaguzi zilizomalizika mwaka jana, sasa uchaguzi umeisha ni kipindi cha kujenga taifa letu.
Tukienda kwa mtindo wa kugawana mbao hatutojenga taifa hili,” alisisitiza diwani huyo wa Vijibweni katika wilaya mpya ya Kigamboni. Alisema ni wakati wa kumsaidia Dk Magufuli kwa kuhamasisha watu wote wanaostahili kulipa kodi walipe kodi hiyo, ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Alisema ili Dar es Salaam ipate maendeleo lazima wananchi hasa wafanyabiashara walipe kodi. “Tunahitaji kujenga madaraja, shule na hospitali. Msidhani Rais ana uwezo wa kutoa fedha mbinguni kwa ajili ya kujenga taifa hili. Lipeni kodi tupate maendeleo,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo (CCM) alisema kwa sasa Jiji la Dar es Salaam lina mameya wanne na wote wamejipanga kufanya kazi kwa maslahi ya wana Dar es Salaam na kuheshimu viongozi wote.
“Usiwe na mashaka na kuhusu utekelezwaji wa Ilani ya CCM katika jiji hili, kwani hata bajeti ya halmashauri zetu zimetumia vigezo vilivyopo kwenye Ilani hiyo,” alisema Chaurembo akimueleza Rais Magufuli.
Akizindua daraja hilo, Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza utaifa mbele badala ya mambo ya vyama, alisema, “Nafikiri kama Wizara ya Ujenzi itakubali kutokana na historia ya daraja hili, wapo viongozi wetu waliofanya makubwa, waliunganisha watu zaidi ya makabila 200, tukapendana bila kubaguana kwa vyama, rangi, lugha wala dini...Na daraja hili halitabagua mtu wa kupita, halitabagua CCM wala Chadema, wote hawa watapita.”

HIACE YATUMBUKIA BAHARINI, YAUA WAWILI

DAR ES SALAAM WATU wawili wamefariki dunia baada ya kutumbukia baharini wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Hiace iliyokuwa imebebwa ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni, Dar es Salaam. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana, wakati kivuko hicho kikipakia abiria katika kituo cha Magogoni. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Brown Mwakalago aliiambia MTANZANIA kuwa lilitokea saa 10 alfajiri ambapo mmoja wa waliofariki dunia ni dada yake, Nice Mwakalago (52) mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya. Akisimulia tukio hilo, Mwakalago alisema walitoka Mbeya kuja Dar es Salaam

Saturday, April 16, 2016

Nusu Fainali ya Uefa Europa League

3330EE6C00000578-0-image-a-15_1460716219507
Droo ya Nusu Fainali ya Uefa Europa League imefanyika na tayari timu nne zilizoingia katika hatua hiyo zimepangwa jinsi zitakavyokutana.
Villarreal imepangwa kuanza mechi ya kwanza ya hatua hiyo kwa kuikaribisha Liverpool wakati ambapo Shakhtar Donetsk itacheza dhidi ya Sevilla.
Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kuchezwa Aprili 28 wakati ambapo mechi za marudio za hatua hiyo zitachezwa Mei 5, 2016.
Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 18, 2016 kwenye Uwanja wa St. Jakob-Park...


RATIBA YA NUSU FAINALI YA EUFA CHAMPIONS LEAGUE HII HAPA

RATIBA YA NUSU FAINALI YA EUFA CHAMPIONS LEAGUE HII HAPA

Tayari ratiba ya nusu fainali ya michuano ya UEFA Champions League imeshatoka baada ya kuchezeshwa draw ya kutafuta nani ataumana na nani kati ya vilabu vinne vilivyosalia kwenye michuano hiyo baada ya Jumanne na Jumatano kushuhudia vilabu vingine vinne vikiyaaga mashindano hayo ikiwa ni pamoja na bingwa mtetezi Barcelona.
Manuel Pellegrini atarejea kwenye klabu yake ya zamani baada ya Manchester City kujikuta ikitakiwa kupambana na miamba ya Hispania Real Madrid wakati Atletico Madrid watakwaana na kikosi cha Pep Guardiola Bayern Munich mechi ambazo zitapigwa April 26/27 na May 3/4.
Atletico Madrid v Bayern unatarajiwa kuwa mchezo wa ina yake uliojaa mbinu na ufundi mwingi kutokana na makocha wa timu hizo kufahamiana vizuri kwasababu walishawahi kuchuana kwenye ligi ya Hispania La Liga wakati Pep akiwa kocha wa klabu ya Barcelona. Kunauwezekano wa kuwepo fainali ya Madrid derby endapo vilabu vyote vya Hispania vitafuzu hatua ya fainali kitu ambacho kilitokea mwaka 2014.
Kitu kingine kizuri ni kwamba, endapo The Bavarians na Manchester City zitafuzu hatua ya fainali, Pep Guardiola atakutana na timu yake atakayoifundisha msimu ujao.

Sunday, April 10, 2016

Njia za Mawasiliano za Jeshi La Polisi Tanzania



NAMBA ZA MAKAMANDA WA POLISI  
MKOA JINA LA KAMANDA NAMBA ZA SIMU  
ARUSHA DCP  LIBERATUS  SABAS 0715 009 912  
MWANZA SACP JASTUS KAMUGISHA 0715 009 949  
KIGOMA SACP FERDINAND E. MTUI 0715 009 915  
RUKWA SACP JACOB MWARUANDA 0715 009 954  
KAGERA SACP AUGUSTINO OLLOMI 0715 009 916  
ILALA SACP LUCAS MKONDYA 0715 009 980  
KATAVI SACP DHAHIRI KIDAVASHARI 0715 009 957  
MOROGORO SACP ULRICH MATEI 0715 009 946  
DODOMA ACP LAZARO MAMBOSASA 0715 009 914  
MBEYA SACP AHMED MSANGI 0715 009 931  
KILIMANJARO ACP WILBROAD MTAFUNGWA 0715 009 923  
PWANI ACP BONAVENTURA MSHONGI 0715 009 953  
MTWARA ACP  HENRY MWAIBAMBE 0715 00 99 48  
SHINYANGA ACP MIKA NYANGE 0767 508 090  
MANYARA ACP FRANCIS MASSAWE 0715 009 929  
NJOMBE ACP PRUDENSIANA PROTAS 0658 376 495   
MARA ACP  RAMADHANI NG'AZI 0715 009 930  
SIMIYU ACP ONESMO   LYANGA 0658 37 64 81  
TANGA SACP LEONARD PAUL 0715 009 963  
LINDI ACP RENATA M. MZINGA (BI) 0715 009 927  
SINGIDA ACP THOBIAS G. SEDOYEKA 0715 009 959  
RUVUMA ACP ZUBERI MWOMBEJI 0715 00 99 56                            
TARIME RORYA ACP  GILLES MROTO 0715 009 964  
GEITA ACP MPONJOLI LOTSON 0658 376 488  
TEMEKE ACP ANDREW SATTA 0715 009 979  
KINONDONI ACP CHRISTOPHER FUIME O715 009 976  
TABORA ACP HAMISI SELEMAN  0715 009 961  
IRINGA ACP PETER KAKAMBA 0715 009 921  
       
       
MAKAMANDA WA VIKOSI NA VYUO VYA POLISI  
JINA LA KIKOSI JINA KAMILI SIMU
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani DCP  Mohamed Mpinga 0754 360 046
kamanda Bohari Kuu la Polisi DCP  Andrian  Magayane 0713 635 425
Mkuu wa Chuo cha Polisi Dar es salaam SACP Fulgence Ngonyani 0715 009 985
Kamanda kikosi cha Anga SACP Modestus Lyimo 0658 37 64 67
Kamanda kikosi cha Wanamaji SACP Mboje  Kanga 0658 481 002
Kamanda kikosi cha Ufundi  SACP Shabani M. Hiki 0713 629 824
Kamanda wa Polisi Tazara   Tazara  SACP Patrick   Byatao 0715 00 30 10
Kamanda wa  kikosi cha Ujenzi Ujenzi  SACP Richard Malika 0658 376 503
Kamanda wa Polisi Reli SACP Simon  Chillery 0658 69 99 96
Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi  SACP Matanga Mbushi 0715 009 972
Mkuu wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya  ACP Mihayo Msikhela  
Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar SACP Deusdedit Nsimeki 0715 009 973
Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)  SACP Frasser Kashai 0719 222 101
Kamanda wa kikosi  cha Polisi Bendi ACP Adelgot Haule 0717 260791
Kamanda wa Polisi viwanja vya Ndege ACP  Martin Otieno 0658 444 488 
Kamanda kikosi cha Polisi Afya  ACP Paulo Kasabago 0713 63 26 91
Kamanda wa  Kikosi cha Kuzuia wizi wa Mifugo              ACP Simon C. Ngowi 0658 37 60 62
Mkuu wa Kikosi cha Mbwa na Farasi SSP DK Eugen Emmanuel 0782 078 503
       
       
       
  MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI  
Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Ernest  Mangu 0789 94 94 95
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi DIGP Abdulrahmani Kaniki 0658 90 01 26
Kamishina wa Fedha na Logistics CP Albert Nyamhanga 0786 02 98 96
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo CP  Nsato Marijani  0658 48 10 03
Kamishina wa Polisi  jamii CP  Mussa Alli Mussa 0782 41 72 47
Kamishina wa Utawala na Utumishi CP Thobias  Andengenye 0688 88 33 73
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Diwani Athumani 0 715 32 34 44
Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi ya Makosa ya Jinai  CP Elice Mapunda 0719 11 40 00
Kamishna wa Intelijensia ya Jinai CP Robert Boaz  0677 88 51 00
Mkuu wa ufuatiliaji na Tathmini  DCP Mpinga Gyumi 0658 27 10 02
Mkuu wa Kitengo cha Miradi ya Maendeleo na Ununuzi DCP Sospeter Kondela 0713  63 58 40
Mkuu wa  Mafunzo   DCP Ally Lugendo 0754 59 44 50
Afisa Mnadhimu Makao  Makuu ya Upelelezi DCP Faustine Shilogile 0786 28 32 55
Mkuu wa operesheni za Polisi DCP Jackson Daniel Nyambabe 0658 47 05 02
Mkuu wa Mipango na Bajeti SACP Francis Massawe  
Mkuu wa Mahusiano ya Kimataifa SACP  Germanus  Muhume 0713 63 36 17
Mkuu wa Interpol    SACP Gustavus Babile 0754  28 89 72
Mkuu wa  Fedha   SACP Ndallo Shihango 0754 50 79 18
Mkuu wa kitengo cha Teknohama ACP Mkungu 0677 00 43 32
Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto ACP Tatu Mfaume  
Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi ACP Akili Mpwapwa 0754 47 08 92
Mhasibu Mkuu  wa Jeshi la Polisi Bw. Frank Msaki 0754 49 42 86
Msemaji wa Jeshi la Polisi SSP Advera Bulimba 0758 00 98 61
Meneja Mkuu Bwalo la Maafisa Oystarbay INSP Antonin Mkundi 0655 83 15 25
Kitengo cha maadili na malalamiko   0732 92 20 68/ 0677 99 99 99
       
       
  KANDA MAALUM YA POLISI DAR ES SALAAM  
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DSM   CP Simon Sirro 0686 28 09 94
Mkuu wa Utawala na Fedha Kanda Maalun   DCP Hezron Gimbi 0677 88 51 03
Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ACP Camilius Wambura 0658 11 11 00
Mkuu wa Kikosi cha Polisi 999 DSM SP  George  Daniel 0713 32 39 99
Simu ya Dharura     111 /112
Chumba cha 999     0787 66 83 06
       
       
  KAMISHENI YA POLISI  ZANZIBAR  
Kamishina wa Polisi Zanzibar CP  Hamdani Makame 0754 41 26 90
Naibu Mkurugenzi  wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar DCP Salum Msangi 0713 37 07 30
       
       
       
  MAKAMANDA WA POLISI MIKOA YA ZANZIBAR
Kaskazini Pemba SACP Hassan Nassiri Ali 0715 00 99 17  
Kusini Unguja ACP Juma Saadi Khamis 0715 00 99 25  
Mjini Magharibi ACP Mkadam Khamis Mkadam 0715 00 99 39  
Kusini Pemba ACP Mohamed S. Mohamed 0715 00 99 24  
Kaskazini Unguja ACP Hassan M. Msangi 0715 00 99 18  
       
     

Rais wa Zanzibar achagua mawaziri 13

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ametangaza Baraza la Mawaziri lenye wizara 13.
Baraza hilo lina sura mpya nane, likiwajumuisha wajumbe kutoka katika vyama vya siasa vya upinzani, wanasiasa mashuhuri visiwani humo, huku naibu mawaziri saba wote wakiwa wageni katika nafasi hiyo.
Akitangaza majina hayo jana, Dk Shein anayeianza awamu ya pili ya utawala wake Zanzibar, alimtangaza Dk Halid Salum Mohammed, ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Donge, kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Katika awamu iliyopita, Dk Halid alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Riziki Pembe Juma, Mwakilishi wa Viti Maalumu, ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, wakati Moudin Castico, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi aliyeteuliwa na Rais, anakuwa Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wazee, Wanawake na Watoto.
Wengine ni Rashid Ali Juma, Mwakilishi wa Jimbo la Amani ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utangazaji, Utalii na Michezo.
Balozi Ali Karume, mmoja wa wanasiasa mashuhuri Zanzibar, ambaye kwa sasa ni Mwakilishi wa Kuteuliwa na Rais, yeye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, huku Salama Aboud Talib, ambaye ni Mwakilishi wa Viti Maalumu na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake nchini (UWT), akiteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira.
Balozi Amina Salum Ali aliyeshika nafasi ya pili, baada ya Rais John Magufuli, katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka jana, yeye ameteuliwa kuwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko.
Wapinzani ndani
Dk Shein pia amemteua Hamad Rashid Mohammed, ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha ADC, ambaye pia amewahi kuwa kiongozi wa ngazi za juu wa CUF, kuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.
Hamad pia ndiye aliyeibuka katika nafasi ya pili katika Uchaguzi Mkuu wa marudio wa Zanzibar kwa kupata kura 6,734 baada ya Rais Shein aliyeibuka na ushindi mnono wa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4.
Waziri huyo wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi alifuatiwa kwa karibu na mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad aliyepata kura 6,076. Viongozi wengine kutoka vyama vya upinzani walioteuliwa katika Baraza la Mawaziri ni Said Soud Said kutoka AFP na Juma Ali Khatib kutoka TADEA, ambao wanakuwa mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu.
Mawaziri wa zamani
Mawaziri wanaoendelea na nyadhifa zao ni Haji Omar Kheir aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za Serikali, huku Issa Haji Ussi Gavu ambaye katika kipindi kilichopita alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, amepanda na kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Baraza la Mapinduzi.
Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi, Haroun Ali Suleiman, ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Katiba, Sheria na Utawala Bora).
Mohammed Aboud Mohamed ambaye katika kipindi kilichopita alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, anaendelea na wadhifa wake huo bila ya mabadiliko, huku Mahmoud Thabit Kombo Jecha, ambaye ni Mwakilishi wa Kiembesamaki akipandishwa kutoka Naibu Waziri wa Afya kuwa waziri kamili wa wizara hiyo.
Naibu Mawaziri Dk Shein ameteua naibu mawaziri saba wote wakiwa ni wapya akiwemo Lulu Msham Khamis kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi na Harusi Said Suleiman kuwa Naibu Waziri wa Afya.
Chum Kombo Khamis, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utangazaji, Utalii na Michezo na Mmanga Mjengo Mjawiri ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Wengine ni Juma Makungu Juma ambaye amechaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Maji, Ujenzi, Nishati na Mazingira, huku Khamis Juma Maalim, akiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na Mohammed Ahmed Salum akiteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.
Waliotemwa
Mawaziri waliotemwa ni pamoja na Dk Mwinyihaji Makame, Mwakilishi wa Dimani ambaye katika baraza lililopita alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Omar Yussuf Mzee.
Mwingine ni Dk Sirra Umbwa Mamboya ambaye katika baraza lililopita alikuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili na katika Baraza la Wawakilishi alikuwa Mjumbe wa Kuteuliwa na Rais, ambaye mwaka huu hakupata uteuzi wowote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee, Rais ataapisha mawaziri wapya na naibu mawaziri leo Jumapili Ikulu kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yao mapya kwa mujibu wa Katiba.
Lawama za SUK
Baada ya kutangaza mawaziri hao, Dk Shein alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa, imekwama kutokana na matakwa ya wananchi na si kikatiba.
Amefafanua kuwa tatizo ni vyama vya siasa ikiwemo CUF, kukacha kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Marudio Machi 20, mwaka huu na kusisitiza hatishwi na uamuzi wa chama hicho na vingine vya upinzani kutoitambua Serikali yake.
“Kukwama kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa si kikatiba ni matakwa ya wananchi ambao waliamua kupigia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi na kushinda katika majimbo yote ya uchaguzi Unguja na Pemba. “Tatizo hapa lipo kwa vyama vya siasa vilivyoamua kususia uchaguzi wa marudio ambao uliitishwa kwa mujibu wa Katiba na sheria za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC,” alisema.
Dk Shein alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ameiongoza kwa miaka mitano, imetekeleza majukumu yake vizuri licha ya kuwepo kwa hitilafu ndogo ndogo alizoziita ni za kawaida.
Pamoja na kuwepo kwa changamoto hiyo ya kukwama kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, iliyotokana na hatua ya makusudi ya CUF ya kutoshiriki katika uchaguzi wa marudio, Dk Shein amesema hatabadilisha vifungu vya Katiba kwa ajili ya kuruhusu na kutoa nafasi ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyokuwa awali.
Kutambuliwa na Mungu
Alisema hababaishwi na kauli za CUF zilizotolewa na Maalim Seif za kutoitambua serikali yake na kusisitiza Serikali yake inatambuliwa na Mungu ambaye ameipa baraka zote pamoja na wananchi wa Unguja na Pemba ambao ndiyo walioipigia kura kwa wingi na kuipa nafasi ya kushika hatamu ya madaraka.
“Serikali yangu inatambuliwa na Mwenyezi Mungu kutokana na kudra zake na anayesema haitambui basi hiari yake, lakini mimi nawapongeza wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, ambao wamenipigia kura za ndiyo kwa ajili ya kunipa ridhaa ya kushika hatamu ya kuongoza dola,” alisema.

Tuesday, March 29, 2016

Agizo la Magufuli kwa MaRC mwisho leo

SIKU 15 alizotoa Rais John Magufuli kwa wakuu wa mikoa, wawe wamejumlisha wafanyakazi wote na kuhakikisha wanaondoa wafanyakazi hewa, zimetimia leo. Baadhi ya mikoa imeanika idadi ya watumishi hewa, waliobainika kupitia uhakiki huo, lakini mingi haijafanya hivyo.
Agizo hilo la Rais Magufuli ni sehemu ya maagizo kadhaa aliyotoa Machi 15 mwaka huu wakati akiwaapisha wakuu hao wa mikoa jijini Dar es Salaam; ambao aliwasisitiza kuwa ili mradi wamekubali kushika wadhifa huo, wameingia kwenye mtego.
Pamoja na majukumu mengine waliyopewa kuhakikisha wanayatekeleza katika uongozi wao, suala la watumishi hewa ni mtego unaowakabili wakuu hao wa mikoa wakipaswa kujinasua nao ndani ya wiki hii ambao siku zilizotolewa zimefika ukomo; Vinginevyo, wataweka rehani nyadhifa zao.
Majukumu mengine ambayo wakuu hao wa mikoa walipewa na Rais wahakikishe wanayatekeleza, ni pamoja na kukabili ujambazi hususan wakuu wa mikoa ya pembezoni inayokabiliwa na tatizo la utekaji magari kiasi cha serikali kuamua kuweka utaratibu wa polisi kuyasindikiza.
Mengine ni kukabili watu wazembe, watendaji wanaowanyanyasa wananchi, njaa, kodi za mazao, migogoro ya ardhi na kuhakikisha wanasimamia mpango wa elimu bure unafanikiwa.
Tangu Rais atoe maelekezo hayo ya kukabili wafanyakazi hewa, mikoa mbalimbali inaendelea na mchakato wa kuhakiki wafanyakazi kwenye idara na taasisi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwataka watumishi kuwasilisha nyaraka mbalimbali ikiwemo barua za ajira.
Katika mchakato huo ambao umezaa matunda kwa kubaini watumishi hewa waliokuwa wakilipwa mishahara, baadhi ya halmashauri zililazimika kufuta huku baadhi ya halmashauri zimeamuru watumishi wake walio masomoni na kwenye likizo, warudi mara moja katika vituo vyao vya kazi kuhakikiwa.
Madudu yaibuliwa Miongoni mwa mikoa ambayo imetoa taarifa za uhakiki ni pamoja na mkoa wa Dodoma, ambao umetajwa kuwa na watumishi hewa 144. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, ameagiza kupelekewa orodha ya watumishi hao na wakati huo huo kupatiwa maelezo kwa nini kuna watumishi hewa na kutaka kupatiwa orodha za watumishi hao.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa aliyehamia Mkoa wa Songwe, Rugimbana alisema uhakiki wa watumishi wa serikali umebaini uwepo wa idadi hiyo ya watumishi hewa .
Mkoa wa Kigoma pia ni miongoni mwa mikoa ambayo taarifa zake za uhakiki zimeshatolewa ambako imebainika kuwapo watumishi hewa 169 kwa kipindi cha mwaka uliopita.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emanuel Maganga amewataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi cha fedha kilichotumika kulipa mishahara watumishi hewa hao 169 ndani ya kipindi hicho cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa huo wa Kigoma, watumishi hewa waliowabaini, wamo waliokwishafukuzwa, waliofariki na wengine wasiokuwa na sifa za kuwa watumishi wa umma.
Maganga ametaka fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwa ajili ya mishahara, zirudi na wakati huo huo wakurugenzi wawafute kwenye orodha ya malipo.
Halmashauri za mkoa wa Kigoma zenye watumishi hewa na idadi yake kwenye mabano ni Kasulu (78), Kigoma (23), Manispaa ya Kigoma Ujiji (29), Buhigwe (11), Uvinza (19), Kibondo (5) na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa yenye watumishi hewa wanne.
Halmashauri ya Kakonko ndiyo pekee isiyo na mtumishi hewa. Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili jana, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo, alisema leo ambayo ndiyo ukomo wa muda aliotoa Rais, atatoa taarifa kamili ya kazi hiyo ya kuhakiki wafanyakazi na kuondoa wafanyakazi hewa watakaokuwa wamebainika.
Ndikilo alisema, ipo timu inayo endelea kufanya uhakiki kwenye wilaya mbalimbali kwa kushirikiana na wakurugenzi wa halmashauri. Likizo zaahirishwa Kwa upande wa mkoa wa Dar es Salaam, Halmashauri ya wilaya ya Temeke ililazimika kuwaita watumishi wake walioko masomoni na likizo kurudi mara moja katika vituo vyao vya kazi wahakikiwe.
Msemaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Joyce Nsumba alisema hivi karibuni uhakiki uliendelea kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Idara ya Afya, Elimu, Fedha na Biashara, Kilimo, Mifugo, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii.
Wakati anazungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Nsumba alisema walishahakiki watumishi 8,000. Sababu za uhakiki Uamuzi wa Rais Magufuli kuamuru ufanyike uhakiki, ulitokana na uchunguzi uliofanywa katika mikoa ya Singida na Dodoma katika halmashauri 14 na kugundulika kwa watumishi hewa 202 wanaolipwa mishahara.
Aliagiza uhakiki kwa watumishi wote katika wizara, mikoa, wilaya, idara,taasisi na Wakala za Serikali ndani ya siku 15. “Sasa niwaombe ndugu zangu wakuu wa mikoa, najua mtakwenda kuwapa maagizo wakurugenzi na wakuu wa wilaya.
Lakini niwape muda, ndani ya siku 15, wawe wamejumlisha wafanyakazi wote, wamewatoa wafanyakazi hewa,” ali waagiza. Rais Magufuli alisema mshahara ujao, ikigundulika kuwapo wafanyakazi hewa kwenye orodha ya malipo, mkurugenzi husika ajihesabu hana kazi na atafikishwa mahakamani.
Vile vile amewaambia mawaziri, hususan Waziri wa Fedha na Mipango aliyekuwapo kwenye hafla hiyo, wakawaeleze watendaji kwenye wizara zao na taasisi mbalimbali wahakikishe wanawaondoa wafanyakazi hewa ndani ya siku 15 na wasipotimiza agizo hilo hatua zitakuwa ni zilezile kwani sheria ni msumeno.
Alisema inasikitisha kuona fedha zinazokusanywa haziendi kwenye miradi inayopangwa, badala yake sehemu kubwa inatumika kulipa mishahara ikiwemo hewa. Alisema kwa ujumla Serikali inalipa mishahara kila mwezi kwa watumishi wake wa umma jumla ya Sh bilioni 549 mpaka bilioni 550.
Alisema kwa hali ilivyo, fedha nyingi zinaishia kwenye mishahara feki. Nawapa Ma-RC siku 15 mhakikishe Wakurugenzi wa halmashauri zote wamejumlisha idadi ya wafanyakazi wote waliopo na kuondoa wafanyakazi hewa katika halmashauri zao,” alisisitiza Rais Magufuli.
Mikoa ya Tanzania Bara ni: Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Geita, Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Singida, Tabora, Pwani, Manyara, Mara, Morogoro na Kilimanjaro